UTANGULIZI.
KRISMASI
ilitokana na neno "Misa ya Kristo" ambayo ni desturi ya Wakatoliki wa
Roma, misa maalum inayofanywa kusherehekea kuzaliwa kwa Kristo.
Krismasi
haikuwa miongoni mwa sherehe za awali za Kanisa la Kikristo. Haikuadhimishwa, kutolewa
heshima, wala kufuatiliwa, na mitume wala katika kanisa la mitume, kwa miaka
300 ya kwanza ya historia ya kanisa, baada ya Ukatoriki kuchukua uongozi wa
kanisa la kwanza la Rumi lililokuwa limeanzishwa awali na Mtume Paulo. Ilikuwa
mwaka 350 A.D. ambapo Papa Julius-I alitangaza kwamba kuzaliwa kwa Kristo kunapaswa
kuadhimishwa "Desemba 25". Historia inaonyesha kuwa Kanisa huko
Yerusalemu lilianza kuadhimisha Krismasi tu mwaka 440 A.D., kufuatia shurutisho
la Ukataliki wa Kirumi.
HISTORIA
YA KALE
Historia
ya zamani inaonyesha kwamba katika tamaduni za kale za kipagani, sio jambo la
bahati mbaya kwamba Desemba 25 pia ilikuwa siku ya kuzaliwa kwa miungu
yao ya kipagani. Sherehe zote za KIBABELI na za KIRUMI ziliambatana na kipindi
cha sherehe cha muda wa siku 5-7 cha shangwe isiyo na kizuizi au ulevi na
uasherati kati ya tarehe 17 na 23 Disemba. Desemba ni wakati wa mwaka ambapo
mchana huanza kurefuka na mwanadamu wa zamani alibarikiwa na “ujenzi upya wa asili”
na kufanya sherehe ya kila mwaka kwa ajili yake.
Tarehe
25 Desemba
ilikuwa Sherehe ya Ushindi wa “Mungu Jua” katika ulimwengu wa Kibabiloni
ya kipagani. Katika Dola la Rumi la zamani, sherehe sawa na hizo zinaweza
kufuatiliwa kwenye Sherehe ya Kirumi iliyoitwa “Saturnalia,” iliyoadhimishwa kwa
lengo la kutoa heshima kwa Saturn, mungu wa mavuno, na Mithras, mungu wa
mwanga. Walifanya sherehe ya sarakasi kipindi hiki cha mwaka. Sherehe zote
mbili zilisherehekewa wakati wa solstice (wakati jua linaonekana upande wa
kaskazini kwa dunia wakati wa majira ya baridi) ya majira ya baridi, kati ya
tarehe 17 na 23 Disemba.
“MJUMBE WA MWISHO ANASEMA NINI KUHUSU “KRISMASI””?
Kwa
wale wanaoamini katika Ujumbe wa Mwisho wa Wakati huu, sote tunatambua kwamba
Mungu alitutumia nabii aliyethibitishwa kwa ajili ya kipindi hiki ili kurudisha
mioyo yetu kwenye IMANI ya Wazee wa Pentekoste na kufundisha kweli ya Biblia.
Wakati huo huo, alitumwa na Mungu kutufunulia MISTARI YOTE iliyojificha katika
Neno, kulingana na agizo la unabii alilopewa kama ilivyoonyeshwa katika Malaki
4:5-6 na Ufunuo 10:7. Kwa hiyo, kutoka mtazamo huu, nataka kuelezea suala hili
lenye utata kuhusu “Krismasi”.
Ufuatao
ni muhtasari wa maelezo muhimu kutoka kwenye mahubiri ya Ndg William Marrion
Branham kuhusu kusherehekea siku ya Krismasi. Unapaswa usome katikati ya
mistari.
1.
KRISTO
ALITUREJEZA KWENYE KIFO CHAKE NA SIO KUZALIWA KWAKE.
Krismasi
haitajwi katika Kitabu chote cha Biblia. Hakuna wakati hata mmoja Yesu aliwahi
kuwarejesha kwenye kuzaliwa Kwake, bali kwenye mauti Yake.
61-1224
- Mabwana, Sisi Tunataka Kumwona Yesu
2.
YESU
KRISTO HAKUZALIWA MWEZI WA DESEMBA; ALIZALIWA MWEZI WA APRILI.
Isingeweza
kuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Kristo. Kamwe isingewezekana kuwa. Angepaswa
azaliwe Marchi ama Aprili, maana Yeye alikuwa ni Mwana-Kondoo. Naye alikuwa ni
mwana-kondoo dume na akazaliwa chini ya kondoo dume, Kondoo. Ilibidi iwe hivyo,
unaona. Na kondoo hawazaliwi Desemba hata hivyo. Kondoo huzaliwa katika majira
ya Kuchipua. Na tena jambo lingine, vilima vya Yuda sasa, kuna futi ishirini za
barafu juu yake. Wachungaji wangaliwezaje kuwa huko nje?
64-1227
- Mnasema Huyu Eti Kuwa Ni Nani?
Sasa, Krismasi si sherehe ya
Kiprotestanti. Ni siku ya
Kikatoliki. Tarehe 25 Desemba ilikuwa miezi na miezi kabla ya ninii yetu…baada
ya…au kabla Bwana wetu hajazaliwa. Bwana wetu alizaliwa Aprili. Lakini
hakuzaliwa Desemba. Ikiwa umekuwa katika Uyahudi, mnamo Desemba, ni baridi
zaidi kuliko hii, kwa hivyo—kwa hivyo unajua Yeye hakuzaliwa Desemba. Na
inaandikwa, ni K-r-i-s-m-a-s-i, misa kwa ajili ya Kristo. Ni misa ya Kristo.
54-1219M - Uponyaji Wa Kiungu
Na jambo lingine, wala Kristo hakuzaliwa tarehe ishirini na tano Desemba.
Isingewezekana Kwake. Kama ulipata kuwa Uyahudi, vilima vimejaa theluji, vibaya
sana kuliko ilivyo hapa. Alizaliwa Aprili wakati maumbile yote yanapochipusha.
Sasa, bali ni mapokeo yao. Na ni kwa nini—kwa nini tunafanya mambo hayo?
Ni kwa sababu tunafuata mapokeo ya wanadamu badala ya amri za Mungu. Hao…Kitu
kama hicho kisingejalisha, bali wanaifanya tu kuwa ni siku ya biashara. Ni
fedheha, aibu kwao kufanya vitu kama hivyo.
60-1204E - Ono La Patimo
3. KRISMASI ILITOKANA NA SHEREHE YA MUNGU
JUA WA WARUMI.
Tunasherehekea siku hii ya 25 ya Desemba kwa ajili ya siku ya kuzaliwa
kwa Kristo, bali, kwa kweli, mtu yeyote anajua ya kwamba haikuwa siku ya kuzaliwa kwa Kristo.
Hiyo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa mungu-jua wa Rumi, ambapo kanisa lilipobadilishwa
kuingia, au, kuingizwa katika Ukatoliki, iliundwa kwenye baraza huko Nikea.
Badala ya hiyo kuwa ya “mungu-jua,” waliifanya siku ya kuzaliwa kwa “Mwana wa
Mungu.” Huo ulikuwa ni wakati, jua, ni kuanzia tarehe 20 mpaka…ninamaanisha
tarehe 21 hadi 25, kwa namna fulani liko kwenye ninii yake…Nasahau ni jina gani
mnaiita, hasa. Ni wakati labda ni mara mbili au mara ya pili linapopita katika
hatua hiyo. Na ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa mungu-jua, nao wakachukua tu
“Mwana wa Mungu” na kufanya hiyo siku ya kuzaliwa Kwake, kuioanisha na desturi
yao ya kikafiri. Na hakuna njia, hata kidogo, hiyo kuwa siku ya kuzaliwa kwa
Kristo.
Asingeweza kuzaliwa wakati huo, kwa sababu Uyahudi uko karibu sawa
kwenye—kwenye ninii…juu kwenye ikweta, kama hii ilivyo, na sisi—sisi tunaona
kwamba, katika Uyahudi, wakati wa baridi kali, tarehe 25 Desemba, una dhoruba
kali ya theluji na baridi. Wachungaji hawawezi kuwa juu ya kilima, na sababu
nyingi isingeweza kuwa.
Halafu basi Yeye alizaliwa kimaumbile, kama vile maumbile mengine yote,
Yeye—Yeye alikuja katika majira ya Kuchipua. Kwa kawaida wakati wana-kondoo
wanapozaliwa, majira ya Kuchipua; na Yeye alikuwa ni Mwana-kondoo. Sasa,
ninaamini, Yeye alizaliwa, mimi mwenyewe, Machi, Aprili, ama mahali fulani
karibu hapo, mwanzoni mwa majira ya Kuchipua.
63-1127 - Ulimwengu Unaporomoka
Tena
Lakini, hii ikiwa ni tarehe 25 Desemba, mbona, wakaifanya siku ya
kuzaliwa, hii ni siku ya kuzaliwa kwa mungu-jua. Mnaona? Baalimu wa
Kirumi, mungu-jua. Mnaona? Nalo jua liko katikati ya mzunguko sasa. Na kuanzia
tarehe 20 hadi tarehe 25 ilikuwa ndiyo wakati sarakasi za Kirumi zilikuwa
zikiendelea, katika kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mungu-jua. Na kwa hiyo
wakasema, “Vema, sasa, kuwafurahisha Wakristo na wapagani pia, tutafanya,
badala ya mungu-jua, Mwana wa Mungu na mungu-jua, pamoja. Kwa hiyo tutazichanganya
zote pamoja na kufanya siku ile ile ya kuzaliwa, na tuifanye iwe tarehe 25.”
Kwa hiyo ilionekana kuwafurahisha makafiri na kanisa la kawaida wakati huo,
kwenye kanisa la kwanza la Kirumi. Ilikuwa ni ninii tu…Ilikuwa tu ni sawa kwao,
kwa hiyo hawakujali. Kwa hiyo wakaifanya siku ya kuzaliwa kwa mungu-jua na ya
Mwana wa Mungu.
61-1224 -Mabwana, Sisi Tunataka Kumwona Yesu
Hili lilifanywa na kanisa Katoliki la Kirumi kabla halijakuwa kanisa
Katoliki huko Roma. Yapata 606 B.K., mahali fulani hapo, ama 306, hasa. Sasa,
tunaona ya kwamba makafiri wa Kirumi walimwabudu Jupita, ambaye ni mungu-jua;
pia walimwabudu Ashtorethi, ambaye alikuwa mungu-mwezi, ama vinginevyo mama
wa…ma—mama wa mbinguni. Vema, kulielezea hili dhahiri, wao walisema ya kwamba
Ashtorethi, ama mungu, mama wa mbinguni hakuwako tena, naye alijiakisi katika
Mariamu. Kwa hiyo ingali ilibaki ni ibada ya sanamu, ikiunganisha Ukristo na
uabudu sanamu.Halafu pia, na waliteseka, ama waliabudu na kuiheshimu siku ya
kuzaliwa kwa mungu-jua wao, ambaye alikuwa ni Jupita.
Ni wakati ambapo jua kutoka tarehe moja Desemba mpaka tarehe ishirini na
tano Desemba, halibadiliki, linapitia kaprikoni yake.
62-1216 -Kuporomoka Kwa Ulimwengu
Lakini basi wakati Ukristo ulipoingizwa katika Urumi na kuchanganywa kule
Nikea, basi walikuwa na mungu-jua, Jupiter, mungu-jua wa Rumi, siku yake ya
kuzaliwa ilikuwa kwenye…kati ya…yapata siku ya ishirini na tano ya Desemba. Kwa
sababu, sarakasi ya Rumi ilianza tarehe ishirini na moja na kuendelea mpaka
tarehe ishirini na tano, ambayo ilikuwa katika kusherehekea siku ya kuzaliwa
kwa mungu-jua. Kwa hiyo kuingiza upagani wa Kirumi katika—katika Ukristo,
walisema, “Hebu tuifanye siku ya kuzaliwa kwa Mwana wa Mungu, ndipo basi
tunaweza sote kukubaliana juu ya hiyo.” Unaona, daima imekuwa ni juu ya mifumo
ya kupatana juu ya Kweli, kila wakati, daima imekuwa hivyo.
63-1216 -Tumeiona Nyota Yake Na Tumekuja Kumsujudia
Pergamo ilialikwa. Vema, walialikwa kwenye karamu baada ya Baraza la
Nikea. Walialikwa kwenye karamu ya Solistasi ya Kipupwe; ambayo inamaanisha,
“jua, kuliabudu jua,” ambalo lilikuwa ni mungu wa kipagani; ambayo ilifanyiwa
mnamo Desemba 21, siku iliyo fupi kuliko zote katika mwaka. Na miaka…Wakati uo
huo haubadiliki mpaka Desemba 25. Makafiri wote waliisherehekea, siku ya
kuzaliwa mungu-jua. Siku ya kuzaliwa kwa mungu-jua ilikuwa ndiyo siku fupi
kuliko zote katika mwaka, Desemba 21. Halafu mtu yeyote aliyepata kuisoma
historia ya makanisa anajua ya kwamba makafiri huabudu kwenye siku hiyo.
Ilikuwa ni sherehe.
Vema, Warumi walikuwa na…walikuwa na michezo mikubwa, sarakasi za Kirumi.
Ni wangapi wameiona hii hapa, chochote ilichokuwa, hapa si muda mrefu uliopita,
waliyoitoa? Ben Hur! Mnaona? Sasa, sarakasi za Kirumi; hizo ndizo Warumi
walizokuwa nazo kwenye siku hiyo ya jua, katika kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa
ya mungu-jua. Mnaona?
60-1207 -Wakati Wa Kanisa La Pergamo
4. KRISMASI SI KITU ZAIDI YA KUWA JAMBO
LA KIBIASHARA
Leo hii, Krismasi inamaanisha pakiti ya sigara za Camels, pakiti ya
Viceroy, chupa ya Four Roses ama Seagramu, zilizofungwa kwenye karatasi nzuri
ya Baba Krismasi.
60-1225 -Zawadi Ya Mungu Iliyofungwa
Lakini imefikia mahali ambapo ni—ni—ni laana kwa watoto wadogo. Maskini
jirani fulani huko chini mtaani anaweza kuwa na mengi, na maskini jamaa huyo
mwingine hana kitu, nao wanaangalia. Na ni—ni kwamba kitu hicho chote ni kosa.
Hivyo tu.
62-1216 -Kuporomoka Kwa Ulimwengu
Na yote ni hadithi za uongo tu, wala Kristo hayumo ndani yake hata
kidogo. Na watu wamegeukia kwenye kununua wiski, na—na kucheza kamari, na
mitindo. Na m—mtu ambaye…mfanyabiashara ambaye anaweza kuuza bidhaa zake msimu
wote wa Krismasi anaweza kuishi mwaka mzima, karibu mwaka mzima uliosalia.
Unaona? Ni likizo kubwa sana, kibiashara. Na maskini watoto wadogo mtaani;
ambao wazazi wao hawawezi ku—kuwatembelea na za—zawadi, kama ile inayotoka kwa
Baba Krismasi, basi wanatembea mtaani, huku maskini mikono yao ni michafu na
macho yao ni mekundu. Na—nachukia kabisa kuiona ikija. Inapaswa kuwa ni siku
yenye uchaji ya kumwabudu Mungu, badala ya kuugua moyo na kuumwa na kichwa na
hayo mambo yanayotendeka. Hakuna kitu kwa Kristo juu ya jambo hilo. Lakini tuko
katikati ya haya yote sasa.
64-1227 -Mnasema Huyu Eti Kuwa Ni Nani?
Katika majuma machache, ama hata sasa hivi, kuna kulungu na akina Baba
Krismasi na—na milio ya kengele na kila namna ya vitu vikining’inizwa, ambayo
ni sherehe ya kipagani. Ni kanuni ya kanisa Katoliki. Watu wakilipa gharama
kubwa na kubadilishana zawadi na vitu kama hivyo, upagani! Krismasi ni siku ya
kuabudu.
Na jambo lingine, wala Kristo hakuzaliwa tarehe ishirini na tano Desemba.
Isingewezekana Kwake. Kama ulipata kuwa Uyahudi, vilima vimejaa theluji, vibaya
sana kuliko ilivyo hapa. Alizaliwa Aprili wakati maumbile yote yanapochipusha.
Sasa, bali ni mapokeo yao. Na ni kwa nini—kwa nini tunafanya mambo hayo?
Ni kwa sababu tunafuata mapokeo ya wanadamu badala ya amri za Mungu. Hao…Kitu
kama hicho kisingejalisha, bali wanaifanya tu kuwa ni siku ya biashara. Ni fedheha,
aibu kwao kufanya vitu kama hivyo. Sherehe ya kipagani! Ni lini Baba Krismasi
alipata kuwa na uhusiano wowote na Yesu? Ni lini sungura wa Pasaka ama kuku
ama…waliotiwa rangi kwa namna fulani ya wino ama chochote kile, ama namna
fulani ya sungura mdogo mweupe walipata kuwa na uhusiano gani na kufufuka kwa
Yesu Kristo? Hivi hamwoni jinsi ulimwengu wa kibiashara…?
60-1204E -Ono La Patimo
Loo, ndugu, dada, jinsi ingekuwa vizuri kama kila mmoja wenu, kama kila
mmoja wetu, sisi, mimi, kama kila mmoja wetu angeweka kando haya yote hapa
mapambo ya Krismasi, unaona, tuachane na huku kote kubadilishana zawadi, mmoja
na mwingine, upuuzi huu wote wa ulimwenguni; na kuondoa tu majivuno yetu na
kuyaweka chini, na kukanyaga kitu hicho chini ya mguu, tuseme, “Bwana Yesu,
niongoze hadi kwenye ile Nuru kamilifu.” Angalia jambo fulani la Kimbinguni
likitendeka. Roho Mtakatifu atakuja kwa njia ya ajabu. Mnaona?
63-1216 -Tumeiona Nyota Yake Na Tumekuja Kumsujudia
Sema, “Ninataka kufuata, ninataka kuifuata Nyota ya Asubuhi, Kristo.
Ninataka kufuata na kumpata Yesu wangu leo hii. Ninataka kuondokea haya yote
hapa mapambo ya Krismasi na kadhalika, kwa sababu siku moja yatateketezwa na
moto usiozimika.” Na wale wote wanaochukuliana nayo, watateketezwa pamoja nayo.
63-1216 -Tumeiona Nyota Yake Na Tumekuja Kumsujudia
Mbona, walianza kununua zawadi za Krismasi miezi kadhaa iliyopita, na ni
kitu gani ila tabia ya kikafiri! Hakuna kitu ambacho ni cha kiungu juu ya jambo
hilo. Loo, wanajaribu kusema, “Kutoa zawadi, kwa mamajusi.” Hilo ni o—oasisi tu
kwa udhuru wa ibilisi. Ukitaka kutoa kitu, ni maisha yako kwa Kristo. Msipeane
mmoja kwa mwingine, mpeni Yeye. Hicho ndicho Yeye alifia. Hilo ndilo kusudi
Lake la kuja.
62-1216 -Kuporomoka Kwa Ulimwengu
5. KRISMASI NI HADITHI NA SHEREHE YA
WAPAGANI.
Tulichukue neno Krismasi. Ni kwa nadra sana unapata kusikia Jina la
Kristo likitajwa. Hulisikii likitajwa. Taa na vivutio vyote viko kwenye Baba
Krismasi, sio kwa Kristo, hata ni vigumu kwa watu kujua Krismasi kweli inahusu
nini. Wameifanya tu ya kikafiri na kuifanya ya kikafiri sana, mpaka yote
imekuwa ni upagani.
61-1224 -Mabwana, Sisi Tunataka Kumwona Yesu
Nikisoma juu ya hadithi za kubuni na hadithi hizi zote za uwongo,
Krismasi yenyewe ni hadithi ya uwongo. Si ninii…Hakuna kitu cha halisi kuhusu
Krismasi. Krismasi hata haikutajwa katika Biblia, kamwe hawakuiabudu siku ya
kuzaliwa kwa Kristo. Hakukuwako na kitu kama hicho. Hilo ni fundisho la sharti
la Katoliki ya Kirumi wala si fundisho la Kikristo, hakuna Maandiko kwake
mahali popote katika Biblia na kwa miaka mia moja ya kwanza baada ya Biblia,
unaona, hakuna lolote kuhusu hilo. Ni hadithi tu ya kubuni. Baba Krismasi,
biashara, kila kitu, kitu hicho chote kimefungamanishwa katika upuuzi mtupu.
61-1217 -Ukristo Dhidi Ya Uabudu Sanamu
Natamani kweli kwamba watu wangeninii, wangeweza kufahamu katika
ulimwengu huu, kwamba Krismasi ni nini hasa. Sasa, neno la kwanza Krismasi ni
ninii—kwa namna fulani ni tamshi la Kikatoliki. Linamaanisha “Ya Kristo…”
K-r-i-s-m-a-s-I, mnaona, “Misa ya Kristo,” mnaona. Ilitengwa ama ilianzishwa na
kanisa la Kirumi. Naye Kristo katu hakuzaliwa tarehe ishirini na tano Desemba
zaidi ya nilivyozaliwa mimi. A-ha. Ni mkusanyiko mtupu kabisa wa fundisho la
sharti. Hivyo tu.
62-1216 -Kuporomoka Kwa Ulimwengu
Nao watu mitaani pamoja na viatu vyao vyenye visigino virefu, na
wanajinyonganyonga huku na huko mitaani, wakikimbia madukani.
Na hapa hivi majuzi mke wangu alikuwa akiniambia, “Mtu fulani alisema,
‘Sijui kile nitakachomnunulia Baba.’ Kasema, “Ndugu yangu atamnunulia kwati la
wiski, na huyo mwingine akasema atamnunulia shampeni.’ Na mmoja akasema, ‘Vema,
nitamnunulia se—seti ya karata.’” Sherehe za Krismasi, upagani, ibada za
ibilisi! Vema.
61-1217 -Ukristo Dhidi Ya Uabudu Sanamu
Leo nilikuwa nikifikiri juu ya makanisa makubwa yakipiga kengele, na
kengele zikilia, na kadhalika namna hiyo; na watu wakienda kanisani, na
kujitayarisha, na wanawake wakinunua kofia zao za Pasaka, na kadhalika. Jambo
hili limefikia wapi? Jamani! Jinsi nisivyoweza kufahamu ambapo sungura ana
uhusiano wo wote na ufufuo, unaona, (la, bwana) jinsi mti wa Krismasi ulivyo na
uhusiano wo wote na Kristo. Ni upagani, rafiki zangu. Tumeacha njia mahali
fulani. Hiyo ni kweli. Lakini sasa mwanamume aliyezaliwa mara ya pili ama
mwanamke anatambua, kwa maana kuna uhai ndani yako, unaokwambia ya kwamba jambo
hilo ni kosa. Hiyo ni kweli? [Kusanyiko linasema, “Amina.”—Mh.]
53-0403 -Ukatili wa Dhambi, Na
Adhabu Iliyogharimu Kuondoa Dhambi Maishani Mwetu
Angalieni, Hawa alikutana na wake. Na vivyo hivyo Hawa wa pili alikutana
na wake huko Nikea, Rumi, ukalipa dhehebu, kanuni za imani, likakubali
mafundisho ya sharti badala ya Neno; likashusha sanamu za kikafiri kama vile
Jupita na kadhalika, na kuwainua Paulo na Barnaba. Na—na likashusha mungu-jua
na mungu-mwezi, Ashtorethi, mungu-mwezi, pamoja na kosha ya duara juu yake, na
kumfanya awe mama wa mungu-jua ambaye ni Jupita. Kisha likabadilisha siku ya
kuzaliwa kwa Yesu kutoka Aprili, ambapo maumbile yote, ambapo alizaliwa chini
ya kondoo dume, maana alikuwa kondoo dume, na likabadilisha hiyo ikawa siku ya
kuzaliwa kwa mungu-jua katika jua kule, ambako inafanya siku moja…Kuna yapata
tu tofauti ya dakika moja katika siku ambapo linapita kwenye tarehe ishirini na
tano Desemba, siku ya kuzaliwa kwa mungu-jua, sio Mwana wa Mungu. Na kila mmoja
wetu hujitumbuiza na Baba Krismasi, na kupamba miti, ukafiri, na mambo kama
hayo, halafu ati tunajiita wenyewe Wakristo? Kanisa la Kikristo lina shida
gani?
64-1212 -Wakati Wa Mavuno
6. SANTA CLAUS ANACHUKUA UTUKUFU BADALA YESU
KRISTO
Utangulizi
Santa Claus au “Father Christmas” ni upotoshaji wa Kidachi wa “Mtakatifu
Nikolaas.” (“Mtakatifu Nicholas” alikuwa askofu wa Kikatoliki wa karne ya 4 wa
Myra huko Asia Ndogo, aliyewapa watoto vitu; alitangazwa kuwa mtakatifu na
Kanisa Katoliki, “akichukuliwa kama rafiki na mlinzi maalumu wa watoto.” Mavazi
mekindu yanatokana na ukweli kwamba maaskofu na makadinali wa Kikatoliki nchini
Italia huvaa nguo nyekundu.) Santa Claus pia alijulikana kama “Kriss Kringle,”
ambayo ni ubadilishaji kutoka Kijerumani cha “Christ Kindl” – Mtoto Yesu.
Santa ni kufuru ndhidi ya Mungu kwa sababu ya kuwekwa kama mbadala wa
Kristo! Mara kwa mara anapewa nguvu za Kimbinguni na sifa za Kiungu ambazo anayestahili
ni MUNGU pekee. Fikiria. Anafanywa kuwa mjuzi wa kila jambo – anajua muda ambao
kila mtoto analala, anaamka, amekuwa na afya mbaya au njema, na anajua hasa
kila mtoto anachotaka (linganisha na Zaburi 139:1-4). Anafanywa kama kwamba
yupo kila mahali – usiku mmoja tu wa mwaka anawatembelea watoto “wema”
ulimwenguni kote na kuwaachia zawadi, anaonekana kuwa kila mahali wakati
uleule. Pia anafanywa kuwa mwenye nguvu zote – ana uwezo wa kumpa kila mtoto kile
anachotaka. Zaidi ya hayo, Santa Claus anafanywa kuwa mwamuzi mwenye mamlaka – hawajibiki
kwa yeyote na hakuna mtu mwenye mamlaka zaidi yake, na anapokuja “mjini,”
anakuja na mfuko wa zawadi kwa wale ambao tabia zao zimekubalika machoni pake.
Lakini hadithi ya Santa Claus inapotosha ukweli wa kuzaliwa kwa Kristo
kwa kuchanganya kidogo ukweli na hadithi ya Santa Claus. Wazazi Wakristo
wanapowadanganya watoto wao kuhusu Santa Claus, wanawaelekeza watoto wao mbali
na Mungu na kuwasababishia kuzingatia mwanaume mnene mwenye mavazi mekundu mwenye
sifa kama za mungu. Haya yote yanamfundisha mtoto kuamini kwamba, kama vile
Santa, Mungu anaweza kuridhika na “matendo mema,” yaliyofanywa ili kupata
kibali chake. Pia, wanafundisha kwamba haijalishi jinsi mtoto alivyokuwa mbaya,
bado atapokea zawadi kutoka kwa Mungu – kama vile Santa hakuwahi kushindwa
kuleta zawadi. Hata katika nyumba za Wakristo waaminifu, Santa Claus amaepachukua
mahali pa Yesu kwenye uelewa na mapenzi ya watoto, akawa roho isiyopingika, alama,
na kitovu cha Krismasi.
Hapa kuna baadhi ya nukuu kutoka kwenye mahubiri ya Ndg Branham kuhusu “Santa Claus”:
Ni kitu gani kilicho cha uwongo kuliko Baba Krismasi? Hapajawahi kuwa na
kitu kama hicho. Kuwaambia watoto uongo, utawajibika kwake kwenye Siku ya
Hukumu.
Si ajabu watu hawajui la kufanya. Wao ni…Wao—wao hawataki kabisa jambo
lililo halisi. Watachukua kitu chochote bandia, bali hawataki kitu kilicho
halisi. Hawazitaki zawadi za Mungu. Loo, jamani! Bila shaka. Hawamtaki Yesu,
hilo ni jambo moja.
60-1225 -Zawadi Ya Mungu Iliyofungwa
Ni Krismasi. Mapambo yote, pilkapilka
zote barabarani, za Baba Krismasi, hadithi ya kubuni ya Kijerumani, fundisho la
sharti la Kikatoliki, hakuna hata sehemu moja yake iliyo kweli. Na inachukua
mahali pa Yesu Kristo, katika mioyo ya Wamarekani wengi sana. Krismasi
haimaanishi Baba Krismasi. Krismasi maana yake Kristo. Si mtu fulani aliye na
kiko kinywani mwake, na akishuka kwenye dohani! Ukiwafundisha watoto wako vitu
kama hivyo, unatarajia wakue wawe nini? Waambie Ukweli, sio kwenye hadithi
fulani za uwongo. Waambie, “Kuna Mungu wa Mbinguni ambaye alimtuma Mwanawe, na
hiyo ndiyo maana ya Krismasi. Naye yuko karibu kuja tena.”
58-1221M
- Yuko Wapi, Mfalme Wa Wayahudi?
Ni
wakati wa Krismasi, ondoeni hawa akina Baba Krismasi na kadhalika, tupilieni
mbali upuuzi huo wa kibiashara. Ulisikia wapi kuhusu Baba Krismasi katika
Biblia? Ni visasili vya Kirumi, havina maana hata kidogo, hakuna kitu kama
hicho. Usiwafundishe watoto wako upuuzi kama huo.
64-1221
-Kwa Nini Ilibidi Iwe Ni Mchungaji Wa Kondoo
Kris
Kringle yuko kote nchini. Alikuwa nani? Mjerumani, mtakatifu wa Kikatoliki
miaka mingi iliyopita, mzee aliyeenda huku na huko akitenda mema. Na siku hizi
imekuwa karibu ni ibada. Hiyo ni kweli. Ni sawa kuwaambia watoto, ama chochote
unachotaka kufanya, nijuavyo mimi. Lakini jambo ni kwamba, ni rahisi sana
kuanguka katika utaratibu huo upande mwingine, na kumsukumia Kristo nje,
misingi halisi ya Kristo, ya Krismasi. Naye mtu anamchukua Kris Kringle badala
ya Krismasi halisi, hiyo ni kweli, “Hakuna nafasi kwa ajili Yake katika nyumba
ya wageni.”
49-1225
-Uungu Wa Yesu Kristo
Ninajua
ya kwamba sisi watu hapa hatuwafundishi watoto wetu hadithi za uwongo kama za
Baba Krismasi. Hatuamini katika kumwambia mtu yeyote uongo, kwa hiyo
hamtawadaganya watoto wenu. Upuuzi kama huo, hicho ni hadithi ya uwongo katika
upeo wake, kwa kitu kama hicho kupachukua mahali pa Kristo katika Krismasi.
Na Krismasi imepoteza…Krismasi si ibada tena; ni sherehe, kunywa, kucheza
karata, karamu za ulevi, ukafiri mtupu tu. Na sio…Nami nilitaka kuninii…Labda
baada ya Krismasi nitazungumza tena juu ya Krismasi, mnaona, kusudi isije
ikawanyima watoto…Lakini huwezi kusema hilo kwa watoto wadogo jinsi hiyo. Hao
huwaona jamaa wadogo usiku wa Krismasi wakipokea zawadi za Krismasi na
kadhalika namna hiyo, hawalielewi. Mnaona? Wananinii tu…hao ni wadogo sana. Na
inatupasa kuwakumbuka, kwamba wao…kwamba wana mambo shirika. Inatupasa
kujishusha tupate kuwakumbuka hao jamaa wadogo.
61-1217 -Ukristo Dhidi Ya Uabudu Sanamu
SWALI: Vipi kuhusu mchezo wa Krismasi katika kanisa la Roho Mtakatifu?
Vema, kama ni kuhusu Kristo, huenda ikawa sawa. Lakini kama inahusu Baba
Krismasi, simwamini huyo. Nimekwisha kuyaacha hayo. Siamini katika Baba
Krismasi kamwe. Ona? Na baadhi ya hivi vitu vidogo vya Krismasi walivyo navyo,
nadhani ni upuzi. Na…Lakini naona wamemwondoka kabisa Kristo katika Krismasi na
kumweka Baba Krismasi mle.
59-1219 -Maswali na Majibu Juu ya Roho Mtakatifu
“Mtazamo sahihi kuhusu kusherehekea ‘msimu wa Krismasi’:”
Hebu nilifanye hili dhahiri. Siamini ya kwamba Yesu angejali ni siku gani
uliiabudia siku ya kuzaliwa Kwake, kama ni tarehe 25, 26, ama kama ni Aprili,
Mei, Juni, Julai, ama wakati wowote iwezao kuwa, mradi tu unaabudu, wewe
mwabudu siku yoyote.
Lakini jambo ndilo hili. Wameuondoa utakatifu kutoka kwenye Krismasi,
kuifanya siyo Krismasi bali, siku ya kuabudu, bali sherehe. Mnaona?
Hatuninii…Mnawasikia watu wakisema, “Tutasherehekea Krismasi.” Hilo ni kosa.
Kamwe hatupaswi kuisherehekea Krismasi. Krismasi ni siku ya kuabudu, sio
sherehe.
61-1224 -Mabwana, Sisi Tunataka Kumwona Yesu
Mungu awabariki. Sio hasa
“Krismasi Njema,” bali baraka za Mungu za Krismasi ziwe juu yenu. Jalia Kristo
wa Kalvari akufiche ndani Yake Mwenyewe, akufunike, akufunike sana na kukuvisha
vazi la Neno Lake, mpaka Neno Lake litakapofanyika mwili ndani yako, ndilo ombi
langu. Mungu awabariki.
61-1224 -Mabwana, Sisi Tunataka Kumwona Yesu
Mnapendana? Geukeni na kupeana mikono ninyi kwa ninyi, mseme, “Mungu
akubariki. Kristo awe pamoja nawe.” Badala ya “Krismasi Njema,” mseme, “Kristo
awe pamoja nawe,” mnapogeuka. Sasa usiondoke, ge—geuka tu, useme, “Kristo awe
nawe.” (Kristo awe nawe.)
49-1225 -Uungu Wa Yesu Kristo
Kwenye mkesha huu wa Krismasi, Bwana, tunashukuru kwa ajili ya kipawa cha
Mungu, kwa Mungu kutupa. Ingawa huu ni baadhi yake, kama tunavyoamini mioyoni
mwetu, ushirikina fulani wa kikafiri wa siku ambayo wamejaribu kuitengeneza na
kuifanya iwe kama misa ya Kristo, lakini sisi hatuji katika njia hiyo ya Baba
Krismasi na miti ya Krismasi na mapambo. Bali tunakuja katika Jina la Bwana
Yesu, kumwabudu Mungu wa Mbinguni, aliyefanyika mwili, mwili kama sisi, na
akakaa miongoni mwetu, apate kutukomboa; na akapata dhihaka ya lile Jina,
akapata dhihaka ya msalaba, akairuhusu taasisi ya kilimwengu kumwua Imanueli,
kusudi Yeye aweze kutuletea Uzima wa Milele.
62-1223 -Dhihaka Kwa Sababu Ya Neno
Na utupe Roho, Roho wa kweli wa Krismasi. Wakati leo…kwamba wakati ambapo
sherehe za kipagani, miti ya Krismasi inaabudiwa, hadithi za uongo za m—mtu
anayeitwa Baba Krismasi, na sungura wetu wa Pasaka, na mitindo mbalimbali
ambayo ulimwengu wa kibiashara umeitumia kwa faida yao, jalia iwekwe kando,
Mungu. Jalia tuingie katika Kristo Neno, kwa kuwa tuliomba katika Jina Lake na
kwa ajili ya utukufu Wake. Amina.
64-1221 -Kwa Nini Ilibidi Iwe Ni Mchungaji Wa Kondoo
WATU WENGI BILA KUJUA WANAVUNJA AMRI KUMI KWA KUSHEREHEKEA KRISMASI:
A: Usitamani – Watoto hujifunza kutamani zawadi za wengine, kutamani vitu vilivyo
kwenye orodha ya Krismasi, kuwachosha wazazi wao kwa muda mrefu katika maduka
ya vitu vya kuchezea, vyote kwa jina la “roho ya Krismasi.”
B:
Usimshuhudie jirani yako uongo. – “Yesu ndiye sababu ya majira/msimu wa krismasi!” ni kilio cha vita vya Wakristo wakati wa
Krismasi,” ingawa ukweli ni kwamba hakuna msingi wa Kibiblia kwa sababu asili
yake ni katika mifumo ya ibada za kipagani. Wakristo wengi wanawaambia uongo
watoto wao kuhusu Santa Claus, “Baba Krismasi”, ambaye “injili” yake ni wokovu
kwa njia ya matendo pamoja na kukubaliwa na thawavu isiyo na masharti. Wazazi
huwadanganya watoto wao kwa miaka mingi kuhusu tabia kama ya Mungu ya Santa
Claus, hali inayowataka kumwamini mungu wa uwongo na muongo, na kisha hawaelewi
kwa nini baadaye watoto wao hawaamini na kutumaini katika Mungu wa kweli, Yesu
Kristo.
C:
Usiibe -
Mienendo ya kutumia pesa wakati wa Krismasi kamwe haiwezi kustahimili mtihani
wa utunzaji wa Biblia. Wakristo, wanapoadhimisha Krismasi, "wanaiiba"
rasilimali za Bwana kwa kutozingatia matumizi sahihi. Wanatumia rasilimali hizi
kwa wingi kwenye vitu visivyo na vya muhimu na visivyo na maana (mara nyingi)
na kutokuwazingatia wale wanaohitaji, wakati huo huo wakidai kamwe hawana pesa
za kutosha kununua vitabu vizuri vya Kikristo, kulipia ghalana za elimu ya
nyumbani, au kununua Biblia kwa watoto wao. (Wakristo pia wangeweza kuwasaidia
wale wenye mahitaji ya kiroho kwa kuwanunulia na kuwapa kanda, vitabu, n.k.) “Tunaiba”
kutoka kwa familia zetu kile wanachohitaji na wanachostahili ili kuwanunulia
zawadi wale wasiohitaji.
D:
Usizini –
Wakati huu “maalum” wa mwaka, mawazo yenye tamaa kwa kweli yanahimizwa. Vijana
wanaruhusiwa kwenda kwenye karamu na kubaki nje hadi muda wa usiku, hivyo
wanakutana na majaribu ambayo vinginevyo hayangekuwepo. Karamu ya Krismasi kwa
watu wazima pia inachochea mawazo mabaya. Maeneo mengine, watu hutumia kofia
zao kubadilishana funguo za vyumba vyao vya hoteli na kufanya vitengo vya
kubadilishana wake. Uzinzi wa kiroho kwa kweli unahimizwa na “msimu” huu.
E:
Usiue – Wivu
na chuki kwa ndugu yangu (ambapo, kulingana na Mathayo 5, ni sawa na mauaji)
kwa sababu ana zaidi kuliko mimi au kwa sababu anapokea zawadi kubwa ya
Krismasi kuliko mimi. Hali hii hutokea sana wakati wa Krismasi ambapo watu wanadhihirisha
ubinafsi, kiburi na tamaa zao.
F:
Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi
upewayo na BWANA, Mungu wako. – Kutoa zawadi za Krismasi si heshima kwa wazazi; neno
“kubadilishana” zawadi (kutoa kwa kutarajia kupokea pia) ni ishara wazi ya
dhihaka zinazoambatana na utamaduni huu.
G: Ikumbuke siku ya Sabato
uitakase. Ikiwa siku ya Krismasi itakuwa Jumapili, makanisa mengi
hurekebisha Siku ya Bwana ya ibada ili kuenanda na ratiba za watu, mara nyingi
kwa kufuta ibaada ya kawaida ya Jumapili jioni. Wengi wa washiriks wake huwa na
shughuli nyingi au wanakuwa wamechoka sana kuhudhuria ibada.
H: Usilitaje bure jina la BWANA,
Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake
bure. “Kristo” na “misa” ni maneno mawili yanayopingana kabisa. Kuyaunganisha
yote mawili ni kumkufuru Kristo. Kuchukua sherehe ya kipagani, kuifanya kuwa ya
Kikristo, na kuiita sherehe ya kuzaliwa kwa Kristo, bila shaka ni kulitaja bure
Jina la Bwana. Zaidi ya hayo, baadhi ya Wakristo wanaojitangaza hutumia dini
(“Siku ya Kuzaliwa kwa Kristo”) kama kificho cha kufunika uovu wa tamaa ya
kujilimbikizia, sanamu, choyo, uchafu, n.k. — sababu zote ni kutoa nafasi kwa matendo
maovu.
I: Usijifanyie sanamu ya
kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini
duniani, wala kilicho majini chini ya dunia - Miti ya Krismasi, Mashada,
Taa… watu wanatilia maanani hizi “picha” wakati wa Krismasi na kuvunja amri
hii. Mungu ametupa “Neno” lake, sio sanamu za kumuabudu (1 Pet. 1:23; Kumb.
4:12, 15-19).
J: Usiwe na miungu mingine
ila mimi. Kutafuta furaha ya kidunia, furaha, na utimilifu kupitia msimu wa
Krismasi kwa Baba Krismasi badala ya uhusiano safi, wa kibinafsi, na wa
Kibiblia na Yesu Kristo, ni dhahiri na rahisi "ibada ya sanamu".
Tufuate kwenye Mitandao